Thursday, January 24, 2013
Watu watatu wafariki dunia katika matukio tofauti
Na Silas Nicodem
Watu watatu wafariki dunia jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti likiwemo la
mwanaume mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka35-40 kugongwa na gari eneo
la Ubungo mataa, wilaya ya Kinondoni tarehe 22 Januari 2013.
Taarifa kutoka jeshi la polisi jijini Dar es Salaam
zimethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa mnamo saa 11:30 alfajiri,
mwanaume amabaye hakufahamika jina lake aligongwa na gari na kufariki papopapo
na kisha dereva wa gari hilo kukimbia. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
hospitali taifa ya Muhimbili.
Sambamba na hilo, jeshi la polisi jijini limethibitisha
kukutwa kwa maiti ya mototo wa kiume ambaye hakufahamika jina lake, anayekadiliwa
kuwa na umri wa miaka 10-15 ikielea katika ufukwe wa bahari ya Hindi, eneo la
bichi ya Paradise wilaya ya Temeke.
Maiti hiyo ilikutwa Jumanne wiki hii mnamo saa 10:00 jioni
ikiwa haina jeraha lolote, mwili wa marehemu umehifadhiwa katitka hospitali ya
Vijibweni, na upelelezi unaendelea.
Katika tukio lingine, huko Chanika Lubakuya wilaya ya Ilala,
Jumanne wiki hii mnamo saa 12:00 jioni, imekutwa maiti ya mwanaume aliyetambulika
kwa jina la Athanas anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 30-35 ikiwa katika
shamba ya minazi.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa pembeni ya maiti hiyo
kulikutwa kamba ya nailoni inayotumika kukweya minazi, huku sehemu ya uso ya
maiti hiyo upande wa kushoto ukiwa umebonyea na kutokwa damu sehemu za pua na
mdomo.
Aidha taarifa ya polisi imesema kuwa chanzo cha kifo hicho
hakikujulikana na mmiliki wa shamba hilo hajafahamika. Maiti imehifadhiwa katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili na uchunguzi bado unaendelea.
Thursday, November 29, 2012
Ligi ya NBA kuoneshwa ATN live
Na Silas Nicodem.
Kituo cha Televisheni ya Agape kwa kushirikiana na Agape Association wanatarajia kurusha mechi za mpira wa kikapu za nchini Marekani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, afisa mahusiano wa ATN/TING, Brian Urassa amesema kuwa lengo la kurusha matangazo hayo ni kuleta hamasa kwa watanzania wenye vipaji vya mpira wa kikapu.
“Tanzania tunawachezaji wawili tu nao ni Martin Ndunguru na Hashim Thabiti ambao ndio maarufu wanaocheza mpira wa kikapu nchini Msarekani, je wengine watahamashishwaje, hivyo ni bora tuanziashe maonesho hayo na vipaji vingine vitajitokeza” alisema Urassa.
Urassa aliongeza kuwa mara nyingi mpira wa miguu ndio umekuwa na mashabiki wengi kuliko mpira wa kikapu hivyo basi kwa kufanya hivi tutaweza kuongeza idadi ya mashabiki wa pmira wa kikapu, na kuweza kuhamasisha timi za kikapu nchini.
Akielezea ratiba za mechi hizo katika ATN zitakazoanza kuoneshwa manamo juma pili ya tarehe 1, Desemba mwaka huu, Urassa amesema mechi zitakuwa zikioneshwa kila siku ya jumapili, saa 9 hadi saa 10 alfajiri na kurudiwa kila jumapili saa 8:30 mchana,na mechi itakayokuwa ya kwnza kuoneshwa ni kati ya Brooklyn dhidi ya Miami.
Wednesday, November 7, 2012
Ajari ya gari yaua wawili
Na John Alex Mganga
DAR ES SALAAM, Watu wawili wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Novemba 5 mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho jijini Dar es salaam.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni CHARLES KENYELLA ameitaja Gari yenye namba za usajili T585AZG, aina ya Land Rover Discover lililokuwa likiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika jina lake.
Gari hilo liliacha njia kutokana na dereva kushindwa kulimudu Gari hilo na kuwagonga wanaume wawili na kusababisha kifo papo hapo.
Kamanda KENYELA amesema watu hao hawakuweza kufahamika kwa mjina yao na kwamba walifahamika kwa mavazi waliyokuwa wamevalia ambapo mmoja alivaa suruali nyeupe ya kitambaa na fulana ya kijivu na mwingine alivaa shati jekundu na suruali ya rangi ya bluu.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi kumtafuta dereva aliyesaabisha ajali hiyo.
Wakati katika tukio jingine moto mkubwa umetokea katika gereji moja maeneo ya Mburahati jijini Dar es salaam na kuteketeza mali zote zilizokuwemo katika gereji hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni CHARLES KENYELLA, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari lenye namba za usajili T836AXT aina ya Mitsubishi Pajero GDI.
Moto huo ulizuka baada ya cheche za moto zilisosababishwa na fundi aliyekuwa akichomelea bomba la X- sous aliyefahamika kwa jina la AZIZI AMIRI na kwamba cheche hizo ziliangukia katika mfumo wa umeme wa gari hilo na kusababisha moto na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwemo ndani ya gari hilo.
Kamanda KENYELA amesema thamani ya mali zilizoteketea katika gari hilo hazikufahamiak na kwamba polisi wanaendelea na upelelezi kubainisha hasara iliyotokana na moto huo. AJ/HK REPORTING

Subscribe to:
Posts (Atom)