Wednesday, November 7, 2012

Ajari ya gari yaua wawili  
Na John Alex Mganga
  
DAR ES SALAAM, Watu wawili wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Novemba 5 mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho jijini Dar es salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni CHARLES KENYELLA ameitaja Gari yenye namba za usajili T585AZG, aina ya Land Rover Discover lililokuwa likiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika jina lake.

Gari hilo liliacha njia kutokana na dereva kushindwa kulimudu Gari hilo na kuwagonga wanaume wawili na kusababisha kifo papo hapo.

 Kamanda KENYELA amesema watu hao hawakuweza kufahamika kwa mjina yao na kwamba walifahamika kwa mavazi waliyokuwa wamevalia ambapo mmoja alivaa suruali nyeupe ya kitambaa na fulana ya kijivu na mwingine alivaa shati jekundu na suruali ya rangi ya bluu.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi kumtafuta dereva aliyesaabisha ajali hiyo.

Wakati katika tukio jingine moto mkubwa umetokea katika gereji moja maeneo ya Mburahati jijini Dar es salaam na kuteketeza mali zote zilizokuwemo katika gereji hiyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni CHARLES KENYELLA, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari lenye namba za usajili T836AXT aina ya Mitsubishi Pajero GDI.

Moto huo ulizuka baada ya cheche za moto zilisosababishwa na fundi aliyekuwa akichomelea bomba la X- sous aliyefahamika kwa jina la AZIZI AMIRI na kwamba cheche hizo ziliangukia katika mfumo wa umeme wa gari hilo na kusababisha moto na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwemo ndani ya gari hilo.

Kamanda KENYELA amesema thamani ya mali zilizoteketea katika gari hilo hazikufahamiak na kwamba polisi wanaendelea na upelelezi kubainisha hasara iliyotokana na moto huo. AJ/HK REPORTING

No comments:

Post a Comment