Watu watatu wafariki dunia katika matukio tofauti
Na Silas Nicodem
Watu watatu wafariki dunia jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti likiwemo la
mwanaume mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka35-40 kugongwa na gari eneo
la Ubungo mataa, wilaya ya Kinondoni tarehe 22 Januari 2013.
Taarifa kutoka jeshi la polisi jijini Dar es Salaam
zimethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa mnamo saa 11:30 alfajiri,
mwanaume amabaye hakufahamika jina lake aligongwa na gari na kufariki papopapo
na kisha dereva wa gari hilo kukimbia. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
hospitali taifa ya Muhimbili.
Sambamba na hilo, jeshi la polisi jijini limethibitisha
kukutwa kwa maiti ya mototo wa kiume ambaye hakufahamika jina lake, anayekadiliwa
kuwa na umri wa miaka 10-15 ikielea katika ufukwe wa bahari ya Hindi, eneo la
bichi ya Paradise wilaya ya Temeke.
Maiti hiyo ilikutwa Jumanne wiki hii mnamo saa 10:00 jioni
ikiwa haina jeraha lolote, mwili wa marehemu umehifadhiwa katitka hospitali ya
Vijibweni, na upelelezi unaendelea.
Katika tukio lingine, huko Chanika Lubakuya wilaya ya Ilala,
Jumanne wiki hii mnamo saa 12:00 jioni, imekutwa maiti ya mwanaume aliyetambulika
kwa jina la Athanas anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 30-35 ikiwa katika
shamba ya minazi.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa pembeni ya maiti hiyo
kulikutwa kamba ya nailoni inayotumika kukweya minazi, huku sehemu ya uso ya
maiti hiyo upande wa kushoto ukiwa umebonyea na kutokwa damu sehemu za pua na
mdomo.
Aidha taarifa ya polisi imesema kuwa chanzo cha kifo hicho
hakikujulikana na mmiliki wa shamba hilo hajafahamika. Maiti imehifadhiwa katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili na uchunguzi bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment